Kuunganishwa wa matawi ya Mkunguni na Lumumba yaliyopo Kariakoo – Dar es Salaam

Wapendwa wateja,

Awali ya yote, Bodi ya Wakurugenzi na Uongozi wa AccessBank Tanzania inawatakia heri ya mwaka mpya 2020 na kuwashukuru sana kwa kuendelea kutumia huduma zetu vizuri. 

Kutokana na maboresho na kuimarika kwa njia mbadala za utoaji wa huduma za kibenki kwa sasa,na ukaribu uliopo wa matawi yetu mawili ndani ya eneo la Kariakoo, (umbali usiozidi kilomita moja), tunapenda kuwataarifu kuwa  tawi la Mkunguni lililopo mtaa wa Mkunguni litaunganishwa na tawi la Lumumba lililopo mtaa wa Lumumba na Kipata Kariakoo, Dar es Salaam kuanzia tarehe 03.02.2020.  Kwa hiyo, huduma zote zitolewazo katika tawi la Mkunguni zitasitishwa rasmi tarehe 02.02.2020.

Wateja wetu wanaohitaji huduma za ndani ya tawi la Mkunguni, watapata huduma hizo katika tawi la Lumumba lililopo katika barabara ya Lumumba na Kipata, Kariakoo kuanzia tarehe 03.02.2020.

Uongozi wa benki unawajulisha ya kwamba hakutakuwa na mabadiliko yoyote kwa akaunti za wateja na pia wateja wataendelea kupata huduma m’badala za kibenki pamoja na huduma ya “Kiotomotela” (ATM).

Uongozi utahakikisha mfumo wa kuhamisha taarifa za wateja wenye asili kutoka tawi la Mkunguni kwenda tawi la Lumumba unafanyika kwa umakini bila kuleta usumbufu wowote.

Mahali lilipo tawi la Lumumba 

Summit Tower

Kiwanja namba 4, Kitalu namba 76, Barabara ya Lumumba na Kipata – Kariakoo

Simu namba +255 784 108 500; Barua pepe: customercare@accessmfb.co.tz

Dar es Salaam, Tanzania.

Saa za Kazi katika tawi la Lumumba

Jumatatu mpaka Ijumaa – Saa 2:30 Asubuhi mpaka Saa 2.00 Usiku

Jumamosi – Saa 2:30 Asubuhi mpaka Saa 8 kamili Mchana

Asanteni Sana kwa ushirikiano wenu.

Uongozi

AccessBank Tanzania Limited